Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:50

Jiji la Nairobi Lajiandaa Kumpokea Obama


Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais wa Marekani, Barack Obama.

Mji mkuu wa Kenya, Nairobi unajiandaa kwa ziara ya mtoto maarufu zaidi wa nchi hiyo, Rais wa Marekani, Barack Obama.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Rais Obama, kutembelea nchi aliko zaliwa baba yake toka alipokuwa rais wa Marekani, na mji mkuu huo wa Kenya upo tayari kwa kila kitu.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika, Gabe Joselow, aliyeko Nairobi, anatuarifu hali ya maandalizi yanavyokwenda na matarajio ya ziara hiyo.

Sehemu zote muhimu zipo katika mkakati wa kusafishwa ikijumuisha mitaa ya mji kabla ya ziara ya rais Obama mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Barabara zinafanyiwa ukarabati, maua yanapandwa, mitaa inapakwa rangi na kamera za usalama zinafungwa maeneo yote muhimu ya jiji kwa kugharamiwa na jiji.

Leah Oyake-Ombis, ambaye ni afisa mkuu wa Mazingira wa jiji la Nairobi, anasema juhudi zinazoendelea si tu za kumkaribisha mgeni mmoja.

“Ninadhani kwa Nairobi na hasa tunavyozingatia huduma za mazingira, ama shughuli hizi unazo ziona tunazifanya kwa sasa, hazikuwa mahsusi ama hatuzifanyi kwa ajili ya ujio wa rais wa Marekani.” Alisema Oyake-Ombis.

Anasema mengi ya maboresho haya yalikuwa tayari kufanyika, lakini yalimetokea kabla ya ujio wa rais wa Marekani.

Hata hiyvo, watu wa Nairobi wanamatumaini rais Obama atazungumzia masuala yatakayo nufaisha nchi na jiji.

“Tukirudi kwa yale yatakayo zungumzwa kwa uhalisia, program zitaanzia hapa Nairobi, kwa hiyo Nairobi ni kama sehemu ya mwanzo ya chochote kizuri kitakacho tokana na ziara.” Aliongeza Oyake-Ombis.

Jiji la Nairobi lina zaidi ya watu milioni 4 ambao wanakabiliana na changamoto mbalimbali kuanzia barabara zenye msongamano mpaka umasikini uliokithiri.

Kuliweka jiji hilo katika hali nzuri ni zaidi ya kupamba kwa kupaka rangi.

Jiji la Nairobi ndilo Wakenya wengi wanalolifahamu.

Lina pilikapilika na linahitaji sana miundombinu. Japokuwa kuna uwezekano kwa rais wa Marekani, kutoona sehemu hii ya mji, wakazi hapa wanasema kufanyika uboreshaji wowote ni jambo zuri.

Mkazi wa jiji hilo James Ony'ncha yeye alionyesha kutatizwa na harakati za usafi unaoendelea jijini Nairobi.

“Wanataka waliweke safi kwa watu ambao wanakuja kutembelea nchi ili ionekane safi. Lakini natamani wandelee kufanya kama kile wanachofanya kwa sasa, tunahitaji kuwe kusafi na kuzuri zaidi kama ilivyokuwa awali.” Alisema Ony'ncha.

Si kila mtu ana shauku. Wengine wanasema fedha zinazotumika kwenye ziara zingeweza kutumika kwa matumizi mazuri.

Simo Ng'ang'a yeye ni mwanajeshi msaafu ambaye alikuwa na maoni tofauti kuhusu gharama zinazotumika kusafisha jiji.

“Kwa mfano sasa kamishna a kaunti ya Nairobi, anajartibu kuandaa yote haya—wote wanajionyesha tu. Anapoteza fedha nyingi. Watu wanahitaji fedha za kuboresha eneo la Mathare, ama Wananchi ambao ni masikini, Kwa hiyo wanapaswa kupewa fedha hizo kuboresha maisha yao." Alisema Ng'ang'a.

Bwana Obama, anaelekea Nairobi kwa ajili ya kushiriki mkutano wa dunia wa wajasiriamali Julai 25.

Japokuwa ziara yake itakuwa fupi tu, wakazi wa mji huo mkuu wanatarajia manufaa yake yatachukuwa muda mrefu baada ya kuondoka.

XS
SM
MD
LG