Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 17:48

Obama Ataka Wamarekani Kuachiliwa na Iran


Rais Barack Obama wa Marekani.
Rais Barack Obama wa Marekani.

Rais Barack Obama jumatano amesema Marekani inaendelea kuishinikiza Iran kuwaachilia wamarekani watatu wanaoshikiliwa na Tehran akiwemo mwandishi wa gazeti la Washington Post na jamaa mwingine anayeaminika kuwepo nchini Iran lakini hajulikani mahali alipo.

Wapinzani kadhaa wanaopinga mkataba wa Iran wanasema kuwa Rais Obama asingeukubali mkataba huo kabla ya wamarekani wote wanne walioshikikiliwa Iran kurudishwa Marekani. Bw Obama amejibu maswali kadhaa kuhusu mambo ya ndani ya Marekani lakini kwa wakati mmoja aliwauliza wanahabari waulize maswali kuhusu Iran kwa matumaini kuwa angeyaweka bayana zaidi na kuliangazia kila swala kwa kina.

Bw Obama ameongeza kusema kuwa unapowasikiliza wapinzani wa mkataba wa Iran, utadhani kuwa Iran inataka kuutawala ulimwengu. Amesema kuwa hata kama Iran hatimaye itaamua kutengeneza silaha za nyuklia baada ya miaka 10 ama 15 ya uangalizi wa kimataifa, Marekani bado itakuwa na ushawishi wa kutosha kuhamasisha mataifa mengine kupinga juhudi hizo.

XS
SM
MD
LG