Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:43

Jeshi la Israeil ladai kufanya mashambulizi Ukanda wa Magharibi likiwalenga wafadhili wa Hamas


Magari ya kijeshi ya jeshi la Israel yakiwa Ukanda wa Gaza.Picha na Reuters
Magari ya kijeshi ya jeshi la Israel yakiwa Ukanda wa Gaza.Picha na Reuters

Jeshi la Israel limesema Alhamis limefanya mashambulizi huko Ukingo wa Magharibi wakilenga watu wanaoshutumiwa walisaidia kulifadhili kundi la wanamgambo la Hamas.

Wakati ikiendelea na kampeni yake ya kuitokomeza Hamas katika Ukanda wa Gaza kwa mashambulizi ya anga na ardhini huko kaskazini, katikati na kusini mwa Gaza.

Taarifa ya Jeshi la ulinzi la Israel imesema limewakamata watu 21 na kuzuia mamilioni ya fedha za Israel katika operesheni huko Ukingo wa Magharibi.

Vikosi vya Israel pia vimefanya mashambulizi ya anga huko Jenin na wanajeshi wa ardhini walifyatua risasi kwa wapalestina wakijibu kile wanajeshi wanasema kuwa watu waliwafyatulia risasi wanaejshi wa Israel.

Shambulizi la ukingo wa magharibi lilikuwa la karibuni kufanyika kufuatia mfululizo wa operesheni ambazo zimefanywa na Israel, ikisema kuwa vikosi vyake vinafanya operesheni za kukabiliana na harakati za kigaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG