Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:02

Shambulizi la Florida: Je, shule za Marekani zitaendelea kuwa salama?


Chuck Schumer
Chuck Schumer

Wanafunzi ambao walinusurika katiika shambulizi la kutumia bunduki la kinyama katika historia ya Marekani wanarejea madarasani Jumatano, wakati serikali kuu na wabunge wakiendelea kujadili jinsi ya kuzuia vijana wadogo kupoteza maisha yao katika kile ambacho watu wote wanakubaliana kuwa shule ziwe sehemu salama katika taifa hili.

Tangia kutokea shambulizi hilo ambapo mtu mwenye silaha aliwauwa watu 17 wiki mbili zilizopita katika shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas masomo yalisitishwa. Mauaji hayo yameibua tena mjadala uliokuwa unaendelea kwa muda mrefu juu ya sheria za kudhibiti silaha.

Spika wa Bunge la Marekani Paul Ryan aliwaambia waandishi Jumanne kuwa “pengo” liliopo katika utaratibu wa kuangalia historia ya wale wanaonunua silaha ni lazima lijazwe na ametaka kuwepo utekelezaji wa “ mabadiliko ya ujumla katika suala zima la afya ya akili.”

“Haya ndio baadhi ya mambo ambayo tutakuwa tunajadili na wanachama wetu, na baraza la seneti na rais ,” Ryan amesema.

Kitu ambacho Ryan na wabunge wengine wa chama cha Republikan ambacho hawajafanya ni kutoa tamko juu ya upigaji marufuku wa silaha zikiwemo silaha za kivita aina ya rifle AR 15 kama ile iliyotumika katika shambulizi la Florida.

“Hatutakiwi kukataza raia wanaofuata sheria kumiliki silaha, sisi lazima tuangalie namna ya kuhakikisha kuwa raia ambao hawastahili kumiliki silaha kimsingi hawana njia ya kupata silaha hizo, amesema Ryan.

Chama cha wamiliki bunduki (NRA) na makundi mengine yanayosimamia haki ya kumiliki silaha wanapinga vikali hatua ya kuzuia Wamarekani kumiliki aina fulani za silaha.

Kwa hivyo viongozi wa Republikan katika Bunge-Congress siyo rahisi kukubaliana na pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuongeza kiwango cha umri wa chini wa kuweza kununua silaha za kivita, pia kupiga marufuku kifaa ambacho kinaitwa “bump Stocks” ambacho kinawezesha silaha hizo za kivita kutupa mamia ya risasi kwa dakika moja, na kushinikiza kuwepo uchunguzi wa kina kwa wanunuzi wa silaha.

Trump ambaye pia ametoa wito kwa walimu kuruhusiwa kubeba silaha madarasani, amesema baada ya kukutana na magava wa nchi nzima Jumatatu kuwa, “nusu yenu mnawaogopa NRA. “Kama [ hiyo NRA] haipo pamoja na nyie, ni lazima tupambane nao mara mojamoja.”

Kwa miaka mingi sasa Wademokrat wamekuwa wakishinikiza kuwepo mfumo wa uchunguzi kamili, ikiwemo taarifa za kwenye mitandao na manunuzi ya silaha.

Kiongozi wa chama cha Demokrat katika Baraza la Seneti Chuck Schumer amesema Jumatatu iwapo Bunge litashindwa kupitisha tu muswada wa ushirikiano wa vyama hivyo viwili kuimarisha mfumo wa kitaifa wa kuchunguza historia ya uhalifu wa mtu anayenunua silaha, itakuwa ni kuemewa kuliko wazi na uzembe wa kushindwa kutekeleza majukumu.”

Wanachama wa chama cha Demokrat katika Bunge wanataka kurejeshwa katazo la silaha za kivita ambalo lilimalizika muda wake muongo mmoja uliopita, lakini viongozi wa chama cha Republikan wanasisitiza kuwa Baraza la Seneti ndilo lenye jukumu la kuchukua hatua zinazofuata.

XS
SM
MD
LG