Ajali hiyo ilitokea huko nchini Mali mwezi Julai 2017, na wataalamu wanasema kuwa ilisababishwa na kukosekana utaratibu sahihi wa mfumo wa ndege wa kujiendesha yenyewe.
Ndege hiyo ilianguka wakati ikisafiri na ujumbe wa kulinda Amani kuelekea eneo la kaskazini la jangwa la taifa hilo la Afrika magharibi na kuwauwa wafanyakazi wawili.
Der Spiegel liliandika wizara ya ulinzi iliarifu kamati ya ulinzi bungeni kuhusu uchunguzi mpya uliopatikana Jumanne. Ilisema utaratibu wa ndege kujiendesha yenyewe ulidhibiti ndege kupaa juu na haijafahamika bado ni nani alipanga utaratibu huo kwenye kompyuta ya ndege hiyo ambao haupo katika ndege nyingine za Tiger.