Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu inasema ukamataji huo ulikuwa sehemu ya msako mjini Brussels ikiwa ni pamoja na ujiani wa Molenbeek. Hakukuwa na maelezio juu ya jinsi watu hao wane wanahusika viopi na shambulizi hilo.
Msemaji wa afisi ya kiongozi wa mashtaka, Eric Van Der Sypt, alimtambulisha mshukiwa huyo katika shambulizi la jumanne kwa herufi O.Z., raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 36 ambaye anaweza kuwa anawasaidia kundi wapiganaji wa Islamic State.
Kemikali na vifaa vingine ambavyo vinaweza kutumika kutengeneza mabomu vimekutwa nyumbani kwa mshukiwa huyo.
Bomu ambalo alikuwa amelificha katika begi lake lilishindwa kuripuka na hivyo halikumjeruhi mtu yoyote. Mshukiwa huyo alipigwa risasi na kuuawa baada ya kujaribu kukabiliana na polisi.
Brussels ilikuwa imetangaza hali ya tahadhari kwa zaidi ya miezi 18 tangu kikundi cha Islamic State kilichokuwa katika mji huo kilipofanya mashambulizi Paris na kuua watu 130 Novemba 2015. Mnamo Machi mwaka jana, mashambulizi katika kiwanja cha ndege cha Brussels na katika stesheni ya treni yameua watu 32.
Washambuliaji wa kujitoa mhanga kwa mabomu waliuwa watu 16 huko katika uwanja wa ndege wa Brussels na baada ya muda mfupi mtu mwengine alijiripua katika stesheni ya treni huko Maelbeek, Brussels na kuua watu wengine 16, Machi 22.