Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:50

Jaji mstaafu ahoji upigaji marufuku shisha Kenya


Vijana wakitumia shisha kama kiburudisho katika kambi ya wakimbizi nchini Sudan.
Vijana wakitumia shisha kama kiburudisho katika kambi ya wakimbizi nchini Sudan.

Jaji Mkuu mstaafu, Dkt Willy Mutunga amehoji hatua ya serikali kupiga marufuku uagizaji, utengenezaji na uuzaji wa shisha nchini Kenya.

Dkt Mutunga amesema Ijumaa kuwa kuna uwezekano kwamba Waziri wa Afya, Dkt Cleopa Mailu alikuwa hajachukuwa ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu Profesa Githu Muigai kabla ya kufanya uamuzi huo.

“kuna uwezekano mkubwa kwamba Waziri wa Afya alikuwa hajataka ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu katika nafasi yake aliyopewa kikatiba na kisheria kabla ya kutangaza katazo hilo. Kwa mtu ambaye haamini juu ya haki ya kuwa na afya ni kitu bora kwa umma ukatazaji wa shisha ni kiburi cha unafiki na udikteta,” Mutunga amesema katika akaunti ya tweet aliyokuwa ameituma.

Wizara ya Afya ilipiga marufuku Jumatano uvutaji wa shisha nchini Kenya.

Katika amri ya serikali iliyochapishwa katika gazette la serikali, Waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, utangazaji na uuzaji wa biashara hiyo ya shisha nchini.

Katika amri ya kisheria iliyotolewa Disemba 28, Dkt Mailu ameonya kuwa mtu yoyote atayekutikana akivunja sheria hiyo ya kupiga marufuku utumiaji wa shisha atatakiwa kulipa faini isiyozidi shilingi 50,000, au kifungo cha muda usiozidi miezi sita, au adhabu zote mbili.”

Na kama kosa hilo la ukiukaji sheria litaendelea, mkosaji atatozwa faini zaidi isiyozidi Shilingi 1,000 kwa kila siku uvunjifu huo wa sheria ulipoendelea kama itakavyo kuwa imeelezwa katika kifungu 163 cha Sheria ya Afya ya Jamii.

“Hakuna mtu atakaye ingiza, tengeneza, uza au kukiweka sokoni kuuzwa, kutumia, kutangaza, kushawishi, kuwezesha au kuwapa moyo watu kutumia shisha nchini Kenya,” imesema sehemu ya amri hiyo.

XS
SM
MD
LG