Israel imesema kuwa ililenga kituo cha wanamgambo, huku wapiganaji 19 wakiuwawa kwenye operesheni hiyo. Wengi wa wakazi milioni 2.3 wa Gaza tayari wamelazimika kuondoka makwao tangu kuzuka kwa vita vya Israel na kundi la Hamas miezi 10 iliopita, baadhi wakilazimika kutoroka kwa zaidi ya mara moja.
Maelfu wamelazimika kujikita kwenye mahema hafifu yasio na huduma za kutosha za kibinadamu, au kuchukua hifadhi kwenye shule kama ilioshambuliwa Jumamosi. Wapalestina wanaoishi Gaza wamesema kuwa hakuna mahala salama palipobaki. Ilani ya karibuni ya kuondoka inajumuisha mji wa Khan Younis, likiwemo eneo ambalo Israel ilitenga la kutolea misaada ya kibinadamu, na ambalo jeshi limesema kuwa roketi zimerushwa.
Israel inalaumu Hamas pamoja na makundi megine ya wanamgambo kwa kujificha miongoni mwa raia, na kisha kufanya mashambulizi. Khan Younis ambao ni mji wa pili kwa ukubwa huko Gaza umeshuhudia uharibifu mkubwa zaidi mwaka huu kufuatia mashambulizi ya anga na ardhini.
Forum