Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, idadi hiyo bado haijadhibitishwa,, na iwapo ni ya kweli, basi itakuwa moja ya kubwa zaidi kutokea ndani ya miezi 10 tangu kutokea kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas. Ofisi ya habari ya utawala wa Gaza imesema kuwa shambulizi hilo limeua zaidi ya watu 100.
Wakati idadi kubwa wa wakazi milioni 2.4 wa Gaza wakiwa wametoroshwa makwao na mapigano hayo, ya Oktoba 7 kutoka kwa Hamas kusini mwa Israel, wengi wao wamechukua hifadhi kwenye majengo ya shule. Tukio la Jumamosi linafikisha jumla ya shule zilizoshambuliwa ndani ya Gaza kuwa 14 tangu Julia 6, ambapo zaidi ya watu 280 wameuwawa kulingana na takwimu za AFP, ambazo pia zilitolewa awali na maafisa wa Gaza.
Serikali ya Gaza imesema kuwa shule ilioshambuliwa ilikuwa imetoa hifadhi kwa takriban watu 250, takriban nusu yao wakiwa ni wanawake na watoto. Alhamisi iliopita idara ya Ulinzi ya Gaza ilisema kuwa Israel ilifanya mashambuli kwenye shule mbili mjini Gaza City na kuuwa zaidi ya watu 18.
Forum