Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 03:29

Iran imewakamata watu 12 ikidai ni majasusi wa Israel


Kamanda mkuu wa kikosi cha mapinduzi nchini Iran Hossein Salami
Kamanda mkuu wa kikosi cha mapinduzi nchini Iran Hossein Salami

Kikosi cha mapinduzi cha Iran Jumapili kilisema kiliwakamata watu 12 kwa kuwa majasusi wanaoshirikiana na Israel ambao walikuwa wanapanga vitendo vya kuvuruga usalama wa Iran.

“Wakati utawala wa Kizayuni na washirika wao wa nchi za Magharibi, hasa Marekani, wameshindwa kufanikiwa katika malengo yao mabaya dhidi ya wananchi wa Gaza na Lebanon, hivi sasa wanataka kuhamisha mzozo nchini Iran kwa kupanga msururu wa njama dhidi ya usalama wa nchi yetu,” taarifa ya kikosi hicho ilisema.

Hali ya taharuki huko Mashariki ya Kati imeongezeka tangu maelfu ya vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na wanachama wa Hezbollah huko Lebanon vilipolipuka katika shambulizi, ambalo lilifanywa na Israel.

Hezbollah na Israel wameshambuliana katika mashambulizi makubwa ya kuvuka mpaka katika mzozo sambamba na vita vya karibu mwaka mmoja vya Gaza.

Kikosi hicho cha mapinduzi kimeongeza kwamba majasusi hao 12 walikamatwa katika mikoa sita tofauti, lakini hakikusema lini walikamatwa.

Forum

XS
SM
MD
LG