Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:03

India yaahidi kuchukua hatua kuzuia vifo vinavyo ongezeka kutokana na athari za joto


Mtu mzima akisumbuliwa na maradhi yanayotokana na joto kali akisubiri kulazwa hospitali ya wilaya ya district Ballia, Jimbo la Uttar Pradesh, India, Monday, June 19, 2023.
Mtu mzima akisumbuliwa na maradhi yanayotokana na joto kali akisubiri kulazwa hospitali ya wilaya ya district Ballia, Jimbo la Uttar Pradesh, India, Monday, June 19, 2023.

Majimbo mawili ya India ambayo yanakabiliwa na joto kali yameripoti vifo kadhaa katika siku za karibuni, serikali ilisema itachukua hatua kuzuia vifo kutokana na athari za joto na kutafuta afueni ya athari ya viwango vya joto vinavyoongezeka. 

Katika miaka ya karibuni, joto kali lililochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa limeongezeka zaidi katika sehemu nyingi za India, wanasema wataalam.

Wiki iliyopita, zaidi ya vifo 100 vimeripotiwa katika majimbo mawili yenye idadi kubwa ya watu huko kaskazini na mashariki, lakini haijulikani iwapo vinahusishwa na joto kali lililovuka nyuzi joto digrii 42 Celsius.

Huko Uttar Pradesh, mamlaka zilisema wanachunguza iwapo vifo vya watu 68 waliokuwa wamelazwa hospitali ya serikali katika wilaya ya Ballia vilihusishwa na joto. Vifo hivyo vilitokea katika kipindi cha siku tano kati ya Alhamisi na Jumatatu.

Huko Bihar, maafisa wamesema kuwa joto linalofukuta liliuwa watu tisa na wengine wengi wamelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayotokana na joto.

Waziri wa Afya wa India, Mansukh Mandaviya, alisema Jumanne kuwa “mipango itafanyika katika kila ngazi kwa ajili ya kulinda maisha ya mtu wa kawaida. Tunataka kuhakikisha hakuna mtu anayekufa kutokana joto.”

Alisema Baraza la Utafiti wa Tiba la India (ICMR) litaandaa mipango ya muda mrefu na mfupi kuweza kupunguza athari hasi za joto. ICMR ni taasisi kuu ya utafiti wa afya India.

Forum

XS
SM
MD
LG