Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 06, 2025 Local time: 19:26

Imarisheni maisha duniani, Museveni awahimiza Wakristo


Siku ya Mashahidi Uganda
Siku ya Mashahidi Uganda

Wakristo nchini Uganda wametakiwa sio tu kujishughulisha na maisha ya milele huko mbinguni lakini pia kuishi maisha bora hapa ulimwenguni.

Wito huo umetolewa na Rais Yoweri Museveni Jumapili wakati wa kuadhimisha Siku ya Mashahidi Uganda katika eneo la Kanisa la Katoliki na Makaburi ya Waanglikani huko Namugonga.

Rais amesema kuwa wakati dini ya Kikristo ikiendelea kufundisha waumini wake kujiandaa na maisha ya mbinguni, wananchi wa Uganda lazima wafanye kazi kwa bidii ili kuweza kuishi maisha bora hapa ulimwenguni.

"Viongozi wa Kikristo wanatuambia kuwa sisi ni wageni hapa duniani na ni wapita njia," ameeleza rais.

Lakini ujumbe huo baadhi ya watu wameuelewa kimakosa na kusema kuwa ilivyokuwa sisi ni wageni; basi hatuna haja ya kuleta maendeleo hapa duniani."

"Marehemu baba yangu, ambaye ni babu wa Amos Kaguta aliishi duniani kwa miaka 96; sasa huyu ni mgeni wa namna gani?

Katika ujumbe huo, Rais pia aliwashukuru Baraza la Muungano wa Dini Uganda, ambalo ameanza kushirikiana nao hivi karibuni kuwaongoza wananchi wa Uganda jinsi ya kunyanyua hali ya kipato cha familia zao.

"Tumekubaliana na Baraza hili, ambao walikuja kunitembelea, kwamba nina mifano ya watu ambao waliweza kutokomeza umaskini kutoka majumbani kwao na kwamba tutashirikiana nao ili waweze kuwahamasisha nyinyi ili muweze kutokomeza umaskini kutoka majumbani kwenu.

Wakati huohuo rais ameyapongeza majeshi ya ulinzi kwa kuimarisha ulinzi wa mamilioni ya mahujaji wakitokea ndani na nje ya nchi ambao walikusanyika huko Namugongo kuadhimisha siku ya Mashahidi.

XS
SM
MD
LG