Afisa mkuu wa bodi ya utalii ya nchi hiyo, Steven Asiimwe, amesema kwamba taasisi hiyo itazindua jengo la makumbusho ya vita ambalo pia litakuwa na habari masaibu ya ukoloni.
Asiimwe amesema kumbukumbu hiyo itaonyesha jinsi utawala wa Amin ulivyowadhulumu na kuwanyanayasa raia katika kipindi cha miaka minane alichokuwa rais.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Asiimwe alisema madhumuni ya hatua hiyo ni kuhifadhi historia ya Uganda.
Aidha, jengo hilo la makumbusho litaangazia matukio ya kundi la Lords Resistance Army (LRA), historia ya kabla na wakati wa ukoloni chini ya Uingereza.
Dikteta Amin alinyakua uongozi mwaka wa 1971. Takriban watu 400,000 wanaaminika kuuawa wakati wa utawala wake.
Aliondolewa mamlakani mwaka wa 1979 na baadaye kupelekwa uhamishoni nchini Saudi Arabia, ambAko alifia mnamo mwaka wa 2003.