Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:01

ICC yamfutia makosa Bemba wa Congo


Jean Pierre Bemba,
Jean Pierre Bemba,

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) Ijumaa imefuta makosa ya uhalifu wa vita na adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela kwa mwanasiasa wa Cong, Jean Pierre Bemba, ikiwa ni pigo kubwa kwa waendesha mashtaka na huenda ikawa na matokeo makubwa kwa siasa za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Jaji Christine Van den Wijingaert amesema Bemba, ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Congo hawezi kuwajibishwa kwa uhalifu uliotendwa na wanajeshi waliokuwa chini ya udhibiti wake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) mwaka 2002 mpaka 2003.

Kwa kuongezea amesema majaji katika kesi hiyo wameshindwa kuangalia juhudi zake za kusitisha uhalifu uliotendwa na Movement for the Liberation of Congo (MLC) mara tu alipofahamu kuhusu hayo na jinsi ilivyokuwa vigumu kwa yeye kuwadhibiti wanajeshi akiwa mbali nao.

Uhalifu wa MLC

“Bwana Bemba hawezi kuwajibishwa kwa uhalifu ulioendeshwa na wanajeshi wa MLC wakati wa operesheni huko Jamhuri ya Afrika ya Kati,” amesema, alipokuwa akisoma maamuzi ya jopo la majaji watano wa rufaa.

Van den Wijingaert amesema juhudi za Bemba kusitisha uhalifu “zimefuta wajibu wake kikamilifu.”

Kufutiwa makosa kwa Bemba ni pigo kubwa sana kwa waendesha mashaka, ambaye kukutwa na hatia kwake ilikuwa moja ya kesi chache ambazo wameshinda tangu mahakama hiyo iundwe mwaka 2002.

Bemba alikuwa mwanasiasa wa juu kukutwa na hatia na mahakama ya kudumu ya uhalifu wa vita, na kesi imeonekana kuweka mfano kwamba maafisa wa siasa na kijeshi huenda wakawajibika kwa vitendo vya wanajeshi waliokuwa chini ya uongozi wao.

Makamu wa rais

Bemba, makamu rais wa zamani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, alikutwa nahatia ya mauaji, ubakaji na vitendo vya utekaji nyara vya wanajeshi wa MLC ambao aliwapeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati kumsaidia rais wa wakati huo Ange-Felix Pattasse.

Bemba hakutolewa haraka Ijumaa licha ya kufutiwa makosa kwasababu alikutwa na hatia ya kuingilia kati ushahidi, na uamuzi wa mahakama ya rufaa katika kesi bado haijakamilika.

Uhsiano na Mobutu Sese Seko

Bemba, mtoto wa kiume wa mfanyabiashara, alikuwa tajiri kutokana na uhusiano wake na kiongozi wa zamani wa Congo, Mobutu Sese seko. Aliingia katika serikali chini ya utawala wa rais wa sasa Joseph Kabila mwaka 2003 kama seheu ya makubaliano ya kushirikiana madaraka ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bemba bado ni mtu maarufu magharibi mwa Congo, ambako chama chake cha MLC ni moja ya harakati kubwa sana za upinzani kwa Kabila, ambaye anatarajiwa kuachia madaraka baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba.

Kwa mujibu wa maoni ya umme nchi nzima yaliyofanya na kundi la utafiti wa Congo la chuo kikuu cha New York mwezi Machi, Bemba atashika nafasi ya tatu endapo atawania urais na atakuwa nyuma ya viongozi wengine wawli wa upinzani kwa silimia ya kura.

XS
SM
MD
LG