Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:54

HRW yadai 2023 ulikuwa mwaka wa ugandamizaji wa haki za binaaadamu na ukatili wa kivita


Wakimbizi kutoka Sudan wakivuka kwenda katika hifadhi nchini Ethiopia Mei 5,2023. Picha na Amanuel Sileshi / AFP.
Wakimbizi kutoka Sudan wakivuka kwenda katika hifadhi nchini Ethiopia Mei 5,2023. Picha na Amanuel Sileshi / AFP.

Mwaka 2023 ulikuwa ni uloshuhudia kuongezeka kwa ukandamizaji wa haki za binaadamu na ukatili wa kivita, hususani katika pembe ya Afrika, kulingana na ripoti mpya ya Human Right Watch iliyochapishwa siku ya Alhamisi.

Kundi hilo la kutetea haki za binaadamu limezilaumu jumuiya za kikanda kushindwa kuchukua hatua za kutosha kuwalinda raia. Serikali za Pembe mwa Afrika zimekabiliana na migogoro mikubwa ya kibinaadamu mwaka 2023. Na kushindwa kudhibiti unyanyasaji uloendelea huko Sudan na Ethiopia, raia walistahimili ukatili mbaya uliofanyawa kwa jina la vita, ripoti ya Human Right Watch imesema.

“Tumeona ukiukwaji wa wazi wa haki za msingi za vita, haki za binaadamu uliofanywa na serikali,” alisema Laetitia Bader, naibu mkurugenzi katika kitengo cha Afrika katika kundi hilo linalotetea haki za binaadamu.

Huko Sudan, vita vilizuka mwezi Aprili mwaka jana, kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Dharura, RSF , na kusababisha vifo vya maelfu na maelfu ya raia pamoja na kusabababisha mamilioni ya watu kupoteza makazi, na kuzua mgogoro wa kibinadamu.

Ripoti hiyo imesema pande zinazozozana mara kwa mara zimekuwa zikitumia silaha nzito katika maeneo yenye watu wengi, badala ya kuuchukulia mgogoro huu kama kipaumbele, serikali zenye ushawishi mkubwa na mashirika ya kikanda yameweza kuleta mafanikio ya muda mfupi kwa kutumia suluhu zinazotoawa mhanga haki za binaadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG