Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 11:35

Hotuba ya Hali ya Taifa yapokewa kwa hisia tofauti Marekani


Rais Donald Trump akimaliza hotuba yake ya hali ya taifa katika Bunge la Congress, Jumanne, Januari 30, 2018.
Rais Donald Trump akimaliza hotuba yake ya hali ya taifa katika Bunge la Congress, Jumanne, Januari 30, 2018.

Wabunge wa Bunge la Congress wameeleza hisia zao juu ya hotuba ya Hali ya Taifa iliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump, na baadhi yao wakipongeza hotuba hiyo.

Wamesema imekuwa na kauli ya kuwaunganisha wanasiasa wa pande mbili na wengine kusema waliona ingelikuwa bora kama angetumia hotuba hiyo kuelezea mambo mahsusi zaidi yanayolikabili taifa.

Mwakilishi wa Republikan Ryan Costello ameiita hotuba hiyo ni chanya ambayo imegusia vipaumbele vya taifa kama vile miundombinu na uhamiaji, na kusema Bunge linahitaji kutumia wiki zinazokuja na miezi ijayo kujazia mapendekezo mapana ya Trump na vielelezo zaidi

β€œPia anafikiria Trump alikuwa ameweka wazi kile ambacho kama taifa tunatakiwa kufanya ili kuendeleza nafasi yetu ya uongozi wa dunia, kuwasaidia washirika wetu, na kuzipa nguvu kauli zinazopinga tawala za kidikteta kote ulimwenguni. Nafikiri ilikuwa ni hotuba nzuri,” Costello amesema.

Seneta wa Chama cha Demokrati Chris Coons amesema alikuwa alikuwa ana matumaini kuwa Trump atawasilisha hotuba yenye ujumbe utaoridhiwa na Republikan na Demokrat na kutoa vielelezo kamili jinsi atavyo boresha miundombinu, akifagilia maslahi ya Marekani duniani kote na kukabiliana na Korea Kaskazini, katika baadhi ya vipengele aliweza kufikisha hilo lakini maeneo mengine aligusia kwa uchache sana.

​
XS
SM
MD
LG