Hatimaye kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye ameruhusiwa kuondoka Nairobi kurundi Uganda baada ya kuzuiliwa kupanda ndege ya Kenya Airways Jumatano asubuhi.
Kulingana na Besigye mwenyewe na habari iliyothibitishwa na shirika la ndege la Kenya Airways kiongozi huyo wa upinzani ataondoka Nairobi na ndege KQ414 saa 11 na dakika 50 jioni kuelekea Entebbe, ikiwa ndege ya mwisho kwa leo kuondoka Nairobi kwenda Entebbe.
Awali Besigye alikataliwa kupanda ndege KQ 410 mapema Jumatano asubuhi baada ya ripoti kuwe serikali ya Uganda imesema haitaruhusu ndege hiyo ya Kenya Airways kutua Entebbe ikiwa na Besigye ndani yake.