Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:46

OSCAR: Filamu ya shambulizi la kigaidi Kenya yateuliwa


Sanamu la Oscar lilioko katika chumba cha Oscar Greenroom huko Los Angeles.
Sanamu la Oscar lilioko katika chumba cha Oscar Greenroom huko Los Angeles.

Filamu iliotengenezwa na mwanafunzi wa Kijerumani inayosimulia shambulizi la kigaidi la basi la Mandera 2015 huko Kenya imeteuliwa katika zawadi ya Oscar.

Filamu fupi, Watu Wote, inasimulia tukio la Mkenya wa kawaida alivyokabiliana na Al Shabaab. Filamu hiyo ilishinda Nairobi Jumanne usiku. Filamu hiyo inaeleza hali halisi iliyotokea Disemba 21, 2015.

Wapiganaji wa Al Shabab walishambulia basi lililokuwa litoka Mandera kuelekea Nairobi, mji ulioko Kenya unaopakana na Somalia. Magaidi walijaribu kuwalazimisha wasafiri Waislam kuwatambua Wakristo. Abiria walikataa.

Filamu hiyo inaonyesha hali ya kuhuzunisha wakati wasafiri hao wakikabiliwa na magaidi hao.

Mwanafunzi huyo anayesomea masuala ya filamu Katja Benrath aliiongoza filamu hiyo kama ni mradi wa kupata shahada yake ya juu huko katika shule ya Uandishi ya Hamburg

“Tumefurahia sana kuteuliwa katika zawadi hii kwani hii ni hatua kubwa kupata kuchaguliwa, kwetu sote, kwa mataifa ya Ujerumani na Kenya.

Kenya, na hasa eneo la mpakani limekuwa likikabiliwa na mashambulizi ya Al Shabaab katika miaka ya karibuni. Filamu ya Watu Wote inaangalia matatizo ambayo yamejitokeza Kenya kutokana na uvunjifu huo wa amani.

Muigizaji wa filamu hiyo ni mwanamke kwa jina la Jua. Anapanda basi hilo ili kumtembelea mama yake ambaye ni mgonjwa. Tunamuona katika filamu hiyo Jua akighadhishwa na mtoto wa Kiislam anayeuza maji. Abiria ambaye ni Muislamu Salah Farah baadae anamuuliza kwa nini amekasirika na Jua anasema mumewe na mtoto wake waliuwawa na magaidi.

Lakini baadae, wakati shambulizi linatokea, Salah anamhami abiria ambaye siyo Muislam. Anawaelezea magaidi ukweli juu ya maadili ya Uislam wa kweli. Hatimaye wanampiga risasi.

Katika ukweli wa yaliyomkuta Salah Farah, ambayo filamu hii inasimulia ni kuwa alikufa kutokana na majeraha kabla ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya shambulio hilo ambalo lilitokea kweli.

Katika filamu hiyo, tunamuona Jua amekaa katika kiti nyuma ya Salah, mkono wake ukimliwaza mtu ambaye amejeruhiwa wakati basi linafanikiwa kukimbia. Muigizaji Adelyne Wairimu amecheza nafasi ya Jua.

XS
SM
MD
LG