Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:39

Fatma Karume aahidi kupigania utawala wa sheria


Rais wa TLS aliyemaliza muda wake Tundu Lissu
Rais wa TLS aliyemaliza muda wake Tundu Lissu

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume mara baada ya kuapishwa mjini Arusha, Tanzania Jumamosi, aliahidi kushirikiana na wenzake kushawishi utawala wa sheria nchini na kuhakikisha TLS inapiga hatua katika nyanja zote.

“Sisi kama wanachama ni muhimu kupigania utawala wa sheria, hatuwezi kwenda mbele bila utawala wa sheria, badala ya kuendesha mambo kwa matamko zaidi wakati Katiba inataka nchi iongozwe kwa sheria zilizotungwa na Bunge,” amesema.

Uchaguzi huo ambao pia ulihusisha wajumbe wa baraza la uongozi lenye wajumbe saba ulifanyika asubuhi Jumamosi kabla ya kuendelea kujadili masuala ya kisheria.

AG hana mamlaka juu ya kanuni hizo

Vyanzo vya habari mjini Arusha vimeripoti kuwa kamati ya chama hicho ilioundwa kujadili uamuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wa kuzifanyia mabadiliko kanuni za uchaguzi wa chama ilisema hakuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko yoyote.

Mjumbe wa baraza la uongozi lililomaliza muda wake, Jeremiah Mtobesya akisoma mapendekezo ya kamati, alisema AG hakuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko bali kuyachapisha kwenye Gazeti la Serikali.

TLS kupeleka shauri Mahakamani

Pia, walipendekeza kufuata njia za kiutawala kuonana na AG au kwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya mamlaka yake kwa TLS.

Akizungumzia mabadiliko yaliyofanywa na AG, Fatma alisema hayana msingi wa kisheria kwa kuwa kanuni za uchaguzi wa TLS zinaanza kufanya kazi baada ya kupitishwa na mkutano mkuu.

Wajumbe wa mkutano walikubaliana na baraza la uongozi kutengeneza kanuni zitakazotamka kuwa si lazima zitangazwe kwenye Gazeti la Serikali ili ziwe halali.

XS
SM
MD
LG