Kwa mujibu wa shirika la habari la AP vikosi vya Eritrea vinashirikiana na vile vya Ethiopia pamoja na makundi shirika yenye silaha, kulingana na msemaji wa TPLF Getachew Reda.
Kupitia ujumbe wa twitter, Reda amesema kwamba Eritrea inatumia jeshi lake lote pamoja na vikosi vya ziada, wakati vikosi vyake vikiwa imara kulinda maslahi yao.
Mamlaka za Tigray kupitia ujumbe wa Jumanne zimeshauri watu wake kuwa tayari kwa vita ambavyo "vitaangamiza kabisa adui zao na kuwapa ushindi wa kudumu."
Mfanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu kwenye mji wa kaskazini mwa Ethiopia wa Adigrat ameambia shirika la habari la AP kwamba vikosi vya Eritrea vimeanza kurusha makombora kwenye maeneo jirani.