Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:54

Siku ya Uhuru wa Habari: 'Mvutano waongezeka katika utoaji habari'


Katika mkutano wa UNESCO confer, Jopo linaloongozwa na Jessica Jerreat, Mhariri wa Uhuru wa Habari wa VOA (katikati) akiwa na kaimu Mkurugenzi wa VOA Yolanda López akiongea katika ufunguzi (Kulia).
Katika mkutano wa UNESCO confer, Jopo linaloongozwa na Jessica Jerreat, Mhariri wa Uhuru wa Habari wa VOA (katikati) akiwa na kaimu Mkurugenzi wa VOA Yolanda López akiongea katika ufunguzi (Kulia).

Dunia inapoadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza Jumanne, shirika la kutetea haki za waandishi habari la Waandishi wasio na Mpaka RSF linasema mvutano unaongezeka kutokana na vurugu kwenye utoaji wa habari.

Ripoti ya shirika hilo lenye makao yake mjini Paris inaonya kwamba kutokana na ukosefu wa kanuni za kusimamia utandawazi wa kutoa habari kwenye mitandao kumekuwepo na ongezeko marudufu la habari za uwongo na propaganda, mivutano katika vyombo vya habari na kusababisha migawanyiko ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi kwenye kiwango cha kimataifa.

Ripoti hiyo imeorodhesha pia hali ya uhuru wa habari katika zaidi ya nchi 180, na kati ya nchi zinazoongoza ni zile za Scandinavia za Norway, Denmark Sweden na Filand pamoja na Estonia.

Na zile zilizoko chini katika orodha ni Korea Kaskazini ikifuatiwa na Eritrea, Iran na Turkmenistan.

Kwa upande wa nchi za Afrika Ushelsheli ndio inaongoza kwa uhuru wa vyombo vya habari na ni miongoni mwa nchi 7 zenye uhuru wa kuridhisha, ikiwa pamoja na Namibia, Afrika kusini, Cape Verde, Ivory Coast Burkina Faso na Sierra Leone

Kwa Afrika mashariki Tanzania imeshuhudia kufunguka kwa uwanja wa uhuru wa habari lakini Kenya kuimarika zaidi katika uhuru huo ikipanda kutoka nafasi ya 102 hadi 62. Ripoti inaeleza Rwanda Burundi hali imekuwa nzuri kidogo lakini Uganda ikishuhudia kubanwa kwa uhuru wa kusema na uhuru wa waandishi habari.

XS
SM
MD
LG