Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Duterte achunguzwa na mahakama ya ICC


Rais Rodrigo Duterte
Rais Rodrigo Duterte

Msemaji wa Rais wa Ufilipino amesema Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imeanza kuchunguza tuhuma za vitendo vya jinai dhidi ya binadamu zilizoelekezwa kwa rais.

Harry Roque amesema Mahakama hiyo ilioko The Hague imemjulisha Rais Rodrigo Duterte kwamba imefungua uchunguzi wa awali juu ya malalamiko yaliofunguliwa mwaka 2017.

Malalamiko hayo yalifunguliwa na wakili mmoja wa Ufilipino kufuatia ukamataji wa kinyama katika vita dhidi ya madawa ya kulevya ambao imeacha watu 4,000 wameuwawa tangu kuingia madarakani Duterte mwaka 2016.

Wanaharakati wa kupigania haki za bindamu wanasema ahadi ya Duterte ya kuwauwa maelfu ya wale wanaojishughulisha na madawa ya kulevya imepelekea polisi kufanya mauaji yaliyovuka mpaka dhidi ya wanaoshukiwa kuwa ni watumiaji na wafanya biashara wa madawa hayo.

Hata hivyo polisi wamekanusha tuhuma hizo za mauaji na wanasisitiza kuwa wamekuwa wakiwauwa washukiwa ambao walikuwa na silaha kwa kujihami wao wenyewe katika operesheni halali ya kupambana na madawa ya kulevya.

XS
SM
MD
LG