Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:38

Pakistan yaitungua ndege ya Iran isiokuwa na rubani


Drone ya Iran - ilionyeshwa na majeshi yake katika maadhimisho ya miaka 37 ya mapinduzi ya Kiislamu, Tehran, Iran, Feb. 11, 2016.
Drone ya Iran - ilionyeshwa na majeshi yake katika maadhimisho ya miaka 37 ya mapinduzi ya Kiislamu, Tehran, Iran, Feb. 11, 2016.

Madai ya Pakistani wiki hii kwamba ilikuwa imeitungua ndege ya Iran aina ya drone inayoruka bila ya rubani tayari yamesababisha mvutano mkubwa kati ya nchi hizo.

Ndege hiyo ilidaiwa kuingia katika anga la Pakistan na tayari imesababisha mvutano mkubwa kuongeza mapigano yaliyoko tayari katika mpaka wao, na pia tofauti za kidiplomasia zinazohusiana na madai ya uchokozi, wachambuzi wamesema.

“Hii ni hali ya kusikitisha kwani itaongeza hali iliyoko tayari ya kutokuaminiana kati ya Pakistan na Iran,” Zubair Iqbal, mchambuzi wa Taasisi ya Mashariki ya Kati kilichoko Washington, ameiambia VOA.

Pande zote za mpaka usioweza kudhibitiwa wa kilomita 900 (maili 560) baina ya Pakistan na Iran, kwa muda mrefu umegubikwa na usafirishaji wa madawa ya kulevya, vikundi vilivyojitenga na harakati za wapiganaji.

Drone hiyo ilianguka siku ya Jumanne kwenye eneo lenye uvunjifu wa amani la Balochistan, jimbo la kusini-magharibi, ambapo waasi na wazawa wa eneo hilo wako tayari kuanzisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya serikali na nchi za jirani.

“Ndege hiyo ilitunguliwa na Jeshi la Anga la Pakistan baada ya kutoweza kutambulika na kuonekana ikiruka kati ya kilomita 3-4 ndani ya himaya ya Pakistani,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amesema katika tamko lake.

Hata hivyo serikali ya Iran imekaa kimya juu ya tukio hilo, japokuwa baadhi ya vyombo vya habari vya Iran vimenukuu magazeti ya Pakistani yakidai shambulizi la ndege hiyo.

Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu wa madhehebu ya Sunni ambao wanaipinga Iran –Jaish al-Adl, au Jeshi la Uadilifu—wamedai kuhusika na shambulizi lililotokea Iran mwezi uliopita ambalo liliwaua walinzi wa mpakani wa Iran 10.

Iran ilijibu hilo shambulizi kwa kuionya Pakistan itawashambulia wapiganaji katika maficho yao ndani ya nchi ndugu ya Kiislam iwapo itashindwa kuwadhibiti wapiganaji hao.

Kutokana na hilo, hatimaye Iran na Pakistan ziliunda tume ya pamoja Mei kutafuta njia ya kuilinda mipaka iwe salama na kuwadhibiti wapiganaji.

XS
SM
MD
LG