Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:10

Maporomoko ya ardhi China: Zaidi ya watu 100 hawajulikani waliko


Wafanyakazi wa uokozi wanaonekana kwenye eneo lililokumbwa na maporomoko nchini China siku ya Jumamosi tarehe 24 Juni, 2017.
Wafanyakazi wa uokozi wanaonekana kwenye eneo lililokumbwa na maporomoko nchini China siku ya Jumamosi tarehe 24 Juni, 2017.

Maafisa wa serikali katika eneo la Kusini Magharibi mwa China, walisema Jumamosi Zaidi ya watu 100 wanaaminika kufunikwa na vifusi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea majira ya asubuhi.

Mamlaka zilisema kuwa maporomoko hayo, ambayo yalisabishwa na mvua kubwa iliyonyesha atika eneo hilo, yaliharibu nyumba 40 katika kijiji cha Xinmo kilicho kwenye jimbo la Sichuan.

Kwa mujibu wa maafisa nchini humo, vifusi, matope na vipande vya mawe kutoka kwenye mlima ulio karibu viliziba sehemu kubwa ya mto unaopitia eneo hilo na kufanya sehemu ya barabara takriban kilomita 1.6 kutopitika.

Taarifa kutoka kwa serikali ya mtaa, ilisema kuwa uokoaji wa dharura umeanza katika eneo lililoathirika na maporomoko hayo ya ardhi.

XS
SM
MD
LG