Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:43

DRC yapokea dozi 50,000 za chanjo dhidi ya Mpox kutoka Marekani


Shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya Mpox ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'Djili mjini Kinshasa, Septemba 5, 2024. Picha ya Reuters
Shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya Mpox ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'Djili mjini Kinshasa, Septemba 5, 2024. Picha ya Reuters

Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema dozi 50,000 za chanjo dhidi ya Mpox kutoka Marekani ziliwasili Jumanne, wiki moja baada ya shehena ya kwanza kutoka Umoja wa Ulaya kuwasili nchini humo.

Watu wazima huko Equateur, Kivu Kusini na Sankuru, majimbo matatu yanayoathirika zaidi, ndio watapewa chanjo hiyo kwanza, kuanzia tarehe 2 Oktoba, Cris Kacita Osako, mratibu wa kamati ya Congo ya kukabiliana na Monkeypox, aliiambia AP.

Wiki iliyopita, shehena ya kwanza ya chanjo ya mpox iliwasili katika mji mkuu wa DRC, kitovu cha mlipuko huo.

Dozi 100,000 aina ya JYNNEOS zilizotengenezwa na kampuni ya Denmark, Bavarian Nordic, zilitolewa kama msaada na Umoja wa Ulaya kupitia idara yake ya majanga ya afya (HERA).

Dozi nyingine 100,000 zilitolewa mwishoni mwa Juma.

Dozi hizo 50,000 zilizotolewa na Marekani ni aina hiyo hiyo ya chanjo ya JYNNEOS.

Dozi hizo 250,000 ni kiwango kidogo sana kati ya dozi milioni 3 ambazo maafisa walisema zinahitajika ili kutokomeza mlipuko wa mpox nchini DRC. Nchi za Umoja wa Ulaya ziliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dozi 500,000 nyingine, lakini ratiba ya usambazaji wa chanjo hizo bado haijawekwa wazi.

Forum

XS
SM
MD
LG