Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:57

Dhoruba yaua watu 35 nchini Afghanistan


Ramani ya Afghanistan
Ramani ya Afghanistan

Dhoruba iliyosababisha mvua kubwa mashariki mwa Afghanistan iliua watu 35 Jumatatu, afisa wa Taliban alisema.

Wengine wengi walijeruhiwa katika jimbo la Nangarhar, kulingana na Sediqullah Quraishi, mkurugenzi wa idara ya habari na utamaduni katika jimbo hilo.

Miongoni mwa waliofariki ni watu watano kutoka familia moja ambao walikufa wakati paa ya nyumba yao ilipoanguka katika wilaya ya Surk Rod, Quraishi alisema.

Ndugu wengine wanne walijeruhiwa.

Alisema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliofariki na kujeruhiwa, na kwamba hali mbaya ya hewa iliharibu nyumba nyingi na mazao katika sehemu tofauti za jimbo.

Aminullah Sharif, mkuu wa hospitali ya jimbo huko Nangarhar, alisema watu 207 waliojeruhiwa walipelekwa kupewa matibabu kutoka Jalalabad, mji mkuu wa Jimbo, na wilaya jirani.

Mapema, shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) lilisema mvua kubwa isiyo ya kawaida nchini Afghanistan iliua zaidi ya watu 300 na kuharibu maelfu ya nyumba, hasa katika jimbo la kaskazini la Baghlan tarehe 10 na tarehe 11 Mei.

Forum

XS
SM
MD
LG