Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:06

Comoro yagubikwa na hali ya wasiwasi


Rais Azali Assoumane
Rais Azali Assoumane

Hali ya wasi wasi imeenea katika visiwa vya Comoro  Jumatano, baada ya polisi kupambana na waandamanaji katika miji mbali mbali, kufuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais Jumanne

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika mji mkuu na kufunga barabara kuu zote za miji muhimu ya visiwa hivyo huku wananchi wakifunga barabara kuzuia wanajeshi kuingia katika miji yao.

Tume huru ya uchaguzi ya Comoro CENI ilitangaza matokeo rasmi ya awali jana jumanne, yanayompatia rais Azali Assoumane, mwenye umri wa miaka 65 ushindi wa asili mia 62.9 na kumrudisha madarakani kwa mhula wanne.

Upinzani umetaka matokeo na uchaguzi kufutwa ukidai kwamba serikali imefanya wizi wa kura kwa kujaza masanduku ya kura na kura zinazomuunga mkono rais Azali.

Msemaji wa serikali Houmed Msaidie akizungumza na shirika la habari la AFP ameulaumu upinzani kwa kuandaa maandamano na kusababisha ghasia.

Forum

XS
SM
MD
LG