Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:24

Coca Cola kuwekeza mabilioni ya dola nchini Nigeria


Picha ya masanduku yenye soda za Coca Cola.
Picha ya masanduku yenye soda za Coca Cola.

Ofisi ya rais wa Nigeria imesema Alhamisi kwamba kampuni ya Coca Cola inapanga kuwekeza dola bilioni moja kwenye operesheni zake nchini humo ndani ya miaka mitano ijayo kufuatia mkutano kati ya wakurugenzi wake na Rais Bola Tinubu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, miongoni mwa wakurugenzi wa Coca Cola waliokutana na Tinubu, ni pamoja na John Murphy ambaye ni rais na mkuu wa fedha, na Zoran Bogdanovic, mkurugenzi mkuu wa HBC ambayo ni mojawapo ya makampuni ya kutengeneza chupa za Coca Cola.

Bogdanovic aliambia Tinubu kwamba tangu 2013, Coca Cola imewekeza dola bilioni 1.5 nchini Nigeria, kama hatua ya kuongeza uzalishaji, usambazaji, mafunzo na maendeleo. Tangazo hilo limekuja baada ya utawala wa Tinubu kushuhudia makampuni kadhaa ya kimataifa kama vile Proctor & Gamble,na Bayer AG, yakiondoka nchini humo, kutokana na uhaba wa fedha za kigeni.

Tinubu ambaye amekuwa ofisini tangu Mei mwaka jana alisema kuwa serikali yake ina azma ya kuweka mazingira bora ya kufanyia biashara. Nigeria yenye zaidi ya wakazi milioni 200, ni soko la kuvutia kwa makampuni mengi ya kimataifa, ingawa uhaba wa fedha za kigeni pamoja na sera ngumu za kufanya biashara, zimevunja moyo baadhi ya wawekezaji.

Forum

XS
SM
MD
LG