Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:55

China yaruhusu wageni kufungua hospitali katika miji tisa


Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping

China Jumapili ilisema itaruhusu kuanzishwa kwa hospitali zinazomilikiwa na wageni katika maeneo tisa ya nchi ikiwemo mji mkuu, huku Beijing ikijaribu kuvutia zaidi uwekezaji wa kigeni ili kukuza uchumi wake unaosusua.

Katika waraka kwenye tovuti rasmi ya wizara ya biashara ya China, ilisema sera hiyo mpya ni mradi wa majaribio uliobuniwa ili kutekeleza ahadi ya Kamati kuu ya chama tawala cha Kikomunisti inayoongozwa na Rais Xi Jinping iliyotolewa katika mkutano wake wa mwezi Julai unaofanyika kila baada ya miaka mitano.

β€œIli kuanzisha uwekezaji wa kigeni kuimarisha maendeleo ya hali ya juu ya sekta zinazohusiana na matibabu za China, na kukidhi vyema mahitaji ya matibabu na afya ya watu, imepangwa kufanya kazi ya majaribio kupanua fursa kwenye sekta ya matibabu,” kulingana na waraka huo.

Mradi huo utaruhusu kuanzishwa kwa hospitali hizo Beijing, Shangai, Nanjing, Suzhou, Fuzhou, Guangzhou, Shenzhen na Hainan, yote ikiwa miji au mikoa yenye utajiri mashariki na kusini mwa China.

Forum

​
XS
SM
MD
LG