Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 16, 2024 Local time: 07:50

China yaharakisha kuimarisha uhusiano na EU kufuatia ushindi wa Trump


Mkuu wa Biashara wa EU Jens Eskelund akiwa mjini Beijing. Ijumaa, Mei, 2024. Picha ya maktaba
Mkuu wa Biashara wa EU Jens Eskelund akiwa mjini Beijing. Ijumaa, Mei, 2024. Picha ya maktaba

China imeongeza juhudi za kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Ulaya baada ya uchaguzi wa Marekani, wakati maafisa wake wa ngazi ya juu, pamoja na vyombo vya habari wakisema kuwa hatua hiyo itakuwa na manufaa kwa Beijing na Brussels.

Wakati mataifa mengi duniani yakijaribu kuangalia ushindi wa Trump utaathiri vipi sera za mambo ya nje za Marekani, wachambuzi wanasema huenda Beijing inalenga kuitenganisha Marekani na Umoja wa Ulaya.

Alicia Bachulska mtaalam kwa sera za mambo ya nje za China kwenye Baraza la Ulaya la Uhusiano wa Kigeni amesema kwamba, “ Ulaya inafahamu vyema kuhusu athari za sera za kigeni na kiviwanda za China kwenye soko moja, pamoja na usalama wa NATO kwenye ukanda wa Mashariki.”

Novemba 9, naibu kiongozi wa Masuala ya Ulaya katika wizara ya mambo ya nje ya China, Cao Lei, alisema kwamba, “kuwa ushindi wa Trump huenda ukabadili mambo,” ni muhimu kwa China kumaliza migawanyiko na kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine. “Hii ni changamoto kwenye uhusiano wa China na EU, Cao Lei alisema wakati wa uzinduzi wa mtandao wa wataalam wa China kuhusu Ulaya, kwenye chuo Kikuu cha Masomo ya Kimataifa mjini Beijing.

Forum

XS
SM
MD
LG