Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 06:33

China, Tanzania na Zambia zasaini makubaliano ya kukarabati reli ya TAZARA


Rais wa China Xi Jinping (Katikati) na mkewe Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Afrika kabla ya hafla ya chakula cha usiku katika Jukwa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) nchini China.
Rais wa China Xi Jinping (Katikati) na mkewe Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Afrika kabla ya hafla ya chakula cha usiku katika Jukwa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) nchini China.

China, Tanzania na Zambia zimesaini makubaliano ya kukarabati reli iliyojengwa miongo kadhaa iliyopita kwa lengo la kuboresha usafiri wa mizigo kwa kutumia njia ya reli na bahari kati nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Shirika la habari la serikali ya China Xinhua, limeripoti kwamba rais Xi Jinping ameshuhudia hafla ya kusaini makubaliano ya kukarabati kilomita 1,860 katika ya China na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, TAZARA.

Marais wa Tanzania na Zambia pia walihudhuria utiaji saini huo. Viongozi hapo wako Beijing kuhudhuria mkutano wa China na viongozi wa nchi za Afrika.

Reli ya TAZARA ilijengwa kati ya m waka 1970 na 1975 kwa mkopo usiokuwa na riba uliotolewa na China.

Reli hiyo inatumika kusafirisha mizigo hasa madini ya almasi naCobalt kutoka Zambia na kupakiwa kwenye meli kwenye pwani ya Tanzania kuelekea masoko ya kimataifa.

Mnamo mwezi Februari, China alipendekeza kukarabati reli hiyo kwa gharama ya dola bilioni 1.

Darzeni ya viongozi kutoka nchi za Afrika wanakutana katika mji mkuu wa China, Beijing.

Mkutano huo unalenga kupata ufadhili kwa miradi mbali mbali ya ujenzi wa miundo msingi na mikataba ya biashara.

Forum

XS
SM
MD
LG