Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 15:32

Chama cha Zuma chajaribu kuzuia Bunge Afrika Kusini kufanya kazi zake


Kiongozi wa chama cha uMkhonto weSizwe (MK) Jacob Zuma (katikati) akiwahutubia wafuasi wake Johannesburg. Picha na Shiraaz Mohamed / AFP.
Kiongozi wa chama cha uMkhonto weSizwe (MK) Jacob Zuma (katikati) akiwahutubia wafuasi wake Johannesburg. Picha na Shiraaz Mohamed / AFP.

Chama cha uMkhonto we Sizwe MK cha rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imewasilisha mashtaka mbele ya mahakama ya katiba kinapojaribu kuzuia kuanza kikao cha kwanza cha bunge jipya siku ya Ijuma.

Lakini kwa upande mwengine chama hicho ambacho kwa mshangao kimeshika nafasi ya tatu kwenye uchaguzi wa May 29, kinadai kwamba kumekuwepo na wizi wa kura na kutishia kususia vikao vya bunge.

Tume huru ya uchaguzi na vyama vingine vimesema uchaguzi ulikua wa huru na haki. Afrika Kusini haina historia ya wizi mkubwa wa kura.

Kwa hivi sasa chama tawala cha ANC kinaendelea na mazungumzo ya kujaribu kuunda serikali ya umoja wa kifa na vyama vingine lakini Zuma amesema MK haitofanya kazi na ANC ya Ramaphosa.

Forum

XS
SM
MD
LG