Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 19:21

Vyama vya Afrika Kusini vyakutana kujadili serekali ya umoja


Vyama vya upinzani vya Afrika Kusini vimekutana Ijumaa na vitaendelea na mazungumzo hadi wiki ijayo kutafakari pendekezo la chama tawala cha African National Congress kuwa sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa.

ANC ilishindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa, lakini baadhi ya vyama vya upinzani tayari vimekataa ombi la chama hicho kwa sababu ya mgawanyiko mkubwa.

Wanachama waandamizi wa chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, au DA, watakutana Jumatatu kujadili mwelekeo wa mazungumzo hayo.

Uongozi wa juu wa chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters, au EFF, pia walifanya mazungumzo Ijumaa. Vyama viko chini ya shinikizo kuhitimisha mazungumzo na kufikia makubaliano ifikapo Juni 16.

Forum

XS
SM
MD
LG