Johnson alisema wabunge wachache walikuwa wanamuunga mkono, ikilinganishwa na wale wanaomuunga mkono Waziri wa Fedha wa zamani Rishi Sunak, katika juhudi za kuwania wadhifa huo.
Hata hivyo, Johnson alisema kwama awali, alikuwa katika nafasi nzuri ya kufaulu katika uchaguzi na wanachama wa Chama cha Conservative, kabla ya Sunak kuonekana kuwa na ufuasi mkubwa zaidi.
Mwanasiasa huyo, ambaye hakuwahi kutangaza rasmi azma yake ya kurejea Downing Street, alitumia wikendi nzima kujaribu kuwashawishi wabunge wa Conservative kumuunga mkono na akasema Jumapili kwamba alikuwa na uungwaji mkono wa 102 kati yao.
Alihitaji kuungwa mkono na wabunge 100 kufikia Jumatatu ili kuendelea hadi hatua inayofuata, ambayo ingempelekea kupambana na Sunak.
Sunak, ambaye kujiuzulu kwake kama waziri wa fedha mwezi Julai kulichangia kuondoka kwa Johnson, alikuwa ameondoa kizingiti cha wabunge 100 waliohitajika kuendelea hadi hatua inayofuata.
Iwapo Sunak atakuwa Waziri Mkuu, atamridhi Truss aliyejiuzulu wiki jana baada ya kukabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa.