Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:03

Boris Johnson anataka tena kuwa waziri mkuu miezi 3 baada ya kutimuliwa


Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson Julai 6, 2022
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson Julai 6, 2022

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson na aliyekuwa waziri wake wa fedha Rishi Sunak wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania wadhifa wa waziri mkuu mpya baada ya kujiuzulu kwa Liz Truss.

Wagombea wa nafasi hiyo wanaendelea kutafuta uungwaji mkono wa kuwa kiongozi wa chama cha Conservative.

Wagombea wanahitaji kupata kura zisizopungua 100 za wabunge wa Conservative.

Kulingana na matokeao ya ukusanyaji wa maoni, chama cha Conservative kinakabiliwa na tishio kubwa la kupoteza wapiga kura wao katika uchaguzi mkuu ujao, huku kikitafuta nani atakuwa waziri mkuu wa tano wa Uingereza katika muda wa miaka sita.

Mshindi wa kinyang’anyiro hicho atatangazwa Jumatatu au Ijumaa wiki ijayo.

Sakata zilizopelekea Johnson kujiuzulu

Boris Johnson, ambaye alilazimika kujiuzlu miezi mitatu iliyopita anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Sunak, katika nafasi ya mbele ya kuwa waziri mkuu wa Uingereza.

Baadhi ya wabunge wa Conservative wamesema kwamba Johnson ana historia nzuri ya kutekeleza mabadiliko yanayohitajika wakati mambo yanapoonekana kutokuwa sawasawa, na kwamba anaweza kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Utawala wa Johnson uligubikwa na sakata za kinidhamu.

Waziri wa biashara Jacob Rees-Mogg amesema kwamba anaunga mkono kurejea kwa Boris Johnson katika uongozi wa Uingereza.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii, wanamuunga mkono Sunak, aliyeteuliwa kuwa waziri wa fedha wakati janga la virusi vya Corona lilipoingia Ulaya. Alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Truss wakati wa kumtafuta waziri mkuu baada ya kujiuzulu kwa Johnson.

Anayetajwa katika nafasi ya tatu ya kinyang'anyiro hicho ni aliyekuwa waziri wa ulinzi Penny Mordaunt.

Mgogoro wa uchumi Uingereza

Liz Truss alijiuzulu kama waziri mkuu wa Uingereza baada ya mpango wake wa uchumi kuharibu utulivu wa kifedha wa Uingereza na kupelekea watu wengi kuwa na matatizo ya kifesha.

Wakati akitangaza kujiuzulu, Truss alisema kwamba hawezi kuendelea kutekeleza mpango wake wa kiuchumi baada ya kutokea mgogoro wa kifedha.

Alilazimika kubadili mpango huo baada ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha ambaye pia ni mshirika wake wa karibu sana kisiasa.

Sunak, ambaye aliukosoa mpango wa uchumi wa Truss, hana umaarufu mkubwa katika chama chake cha Conservative. Aliongoza kampeni iliyopelekea kuondolewa madarakani Boris Johnson.

Waziri mkuu mpya wa Uingereza atakabiliwa na wakati mgumu kujenga uchumi ambapo tayari kuna mfumuko wa bei uliofikia asilimia 10, nafasi za ajira zimepungua na gharama ya maisha imepanda.

Hakuna mgombea aliyetangaza rasmi nia ya kujaza nafasi inayoachwa na Liz Truss lakini chama cha Conservative kimeanza kumtafuta waziri mkuu mpya.

XS
SM
MD
LG