Chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa mashine za kuzima moto ziliwashwa katika jengo lililokuwa linashukiwa kuwa na bomu na watu wanaoishi katika nyumba hizo katika ghorofa mbili walikuwa tayari wameondolewa.
Mji huo bado umekuwa na wasiwasi baada ya tukio la mlipuko kwenye eneo la stesheni ya reli ya St Petersburg Jumatatu, ambalo liliua watu 14.
Mlipuko katika upande wa Kusini mwa Russia katika mji wa Rostov-on-Don mapema Alhamisi, ulimjeruhi mtu mmoja, chanzo cha polisi kimeiambia TASS.
Kituo cha Televisheni cha REN-TV kimewataja mashuhuda wakisema kwamba mlipuko huo ulitokea karibu na shule kwenye mtaa wa Sadovaya na kuwa mfanyakazi aliyekuwa anafanya matengenezo alijeruhiwa katika mlipuko huo.