Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:32

Bobi Wine asisitisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Museveni


Rais Yoweri Museveni (Kushoto) na Bobi Wine.
Rais Yoweri Museveni (Kushoto) na Bobi Wine.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amesema mapema Jumatatu amefuta kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa Januari kwa madai kuwa mahakama ya juu inaegemea upande mmoja.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, Bobi Wine ameayasema hayo wakati akiongea na wanahabari mjini Kampala.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 39 alipinga matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa yalijawa na udanganyifu pamoja na ghasia kwenye sehemu nyingi za nchi hiyo.

Museveni ambaye ametawala Uganda tangu mwaka 1986 baada ya kuwa kiongozi wa waasi alitangazwa mshindi kwenye zoezi hilo la Januari 14 akiwa na asilimia 59 ya kura zilizopigwa mbele ya Wine aliepata asilimia 35 ya kura.

Msemaji wa mahakama Solomon Muyita hata hivyo amesema kuwa mahakama itamjibu Wine wakati atakapo toa ombi la kufuta kesi hiyo kwa njia rasmi kupitia mawakili wake, akiongeza kuwa alichofanya kwa sasa ni kutoa matamshi ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG