Wanadiplomasia hao wamewalaumu wanamgambo wa Hamas na kuunga mkono haki ya Israel kujitetea na kutoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda kwa manufaa ya kibinadamu ili kuingiza misaada kwa raia wenye shida kubwa huko ukanda wa Gaza.
Blinken alikutana na wenzake wa Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani , Japan, na Italy mjini Tokyo kabla ya kutoa taarifa kuhusu msimamo wao wa pamoja.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alikuwa na haya ya kusema: “ Tumekuwa na majadiliano ya kina, kuhusu hatua ambazo tunachukua kutatua shida kubwa iliyopo kwenye eneo.
Wote tumekubaliana kwamba kusitishwa mapigano kwa muda kwa manufaa ya kibinadamu kutasaidia kuwalinda raia wa palestina , kuongeza uingizaji wa misaada ya kibinadamu , kuwaruhusu raia wetu na raia wa kigeni kuondoka na kusaidia kuachiliwa kwa mateka."
Blinken alisema pia atatoa taarifa kwa wenzake kuhusu mazungumzo na viongozi wa Israel kuhusu kusitishwa na hatua za kupunguza madhara kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Amesema Israel imerejea mara kadhaa kusema kuwa haiwezi kurudi nyuma hadi Octoba 6 siku moja kabla ya shambulizi la wanamgambo wa Hamas.
Forum