Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:22

Blinken amefanya ziara ya kushtukiza leo Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Mamlaka ya Palesrina Mahmoud Abbas. Picha hii imetolewa na ofisi ya habari ya Mamlaka ya Palestina (PPO). November 5, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Mamlaka ya Palesrina Mahmoud Abbas. Picha hii imetolewa na ofisi ya habari ya Mamlaka ya Palestina (PPO). November 5, 2023.

Ziara ya Blinken ambayo haikutangazwa ya mjini Ramallah huko Ukingo wa Magharibi ilifuatia mkutano wake wa Jumamosi na viongozi wa kiarabu mjini Amman, Jordan. Pia alitarajiwa kuitembelea Uturuki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alifanya ziara ya kushtukiza Jumapili huko Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel, ambako alikutana na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Palestina.

Ziara ya Blinken ambayo haikutangazwa ya mjini Ramallah huko Ukingo wa Magharibi ilifuatia mkutano wake wa Jumamosi na viongozi wa kiarabu mjini Amman, Jordan. Pia alitarajiwa kuitembelea Uturuki. Israel imesema tangu ilipoanzisha vita dhidi ya Hamas hapo Oktoba 7, “zaidi ya malengo 2,500 ya kigaidi yameshambuliwa”.

Malengo hayo yalishambuliwa, Israel imesema, kutokaba na “harakati za mchanganyiko” za vikosi vya ardhini vya Israel, anga na majini. Jeshi la Israel limesema katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wake wa Telegram kwamba “Usiku kucha, vikosi vya IDF vilielekeza ndege kushambulia kambi ya kijeshi ya Hamas yenye vituo vya kamandi na udhibiti, vituo vya uchunguzi, na miundombinu ya ziada ya magaidi”.

Kampeni dhidi ya Hamas ilizinduliwa baada ya shambulio la kushtukiza la Hamas lililosababisha vifo vya zaidi ya Wa-Israeli 1,400 na zaidi ya watu 200 walishikiliwa mateka.

Forum

XS
SM
MD
LG