Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:39

Biden kutangaza uwekezaji wa dola milioni 600 kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden, Jumatatu atazuru mji wa Palo Alto, jimbo la California, na kutangaza zaidi ya dola milioni 600 za uwekezaji wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kusaidia jamii za pwani kote nchini , afisa wa White House alisema Jumapili.

Uwekezaji huo utafadhiliwa kupitis miswada ya hali ya hewa na miundombinu ya Biden na utajumuisha mradi wa dola milioni 575 za kupambana na kuongezeka kwa maji ya bahari, mawimbi ya dhoruba na vimbunga, alisema afisa huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Pia mpango huo utajumuisha uwekezaji wa dola milioni 67 kwa jimbo la California kufanya gridi yake ya umeme iwe ya kisasa, ili kupunguza athari za matukio ya hali ya hewa kali kama vile moto wa nyika.

Biden alitia saini mswada wa dola bilioni 430 mwezi uliopita wa Agosti ambao ulitajwa kuwa mkubwa zaidi wa hali ya hewa katika historia ya Marekani.

Akiwa California, Bidan pia atchangisha pesa za kampeni kutoka kwa wafadhili wa sekata za teknolojia na hali ya hewa , wakati akiwa mbioni kukusanya zaidi ya dola bilioni moja kwa ajili ya kapeni ya kutaka kuchaguliwa tena.

Forum

XS
SM
MD
LG