Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:36

Hatua zaidi zahimizwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa


Viongozi wa dunia waliokusanyika kwa mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa COP21 mjini Paris, Ufaransa.
Viongozi wa dunia waliokusanyika kwa mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa COP21 mjini Paris, Ufaransa.

Obama alisema ameshuhudia binafsi athari za mabadiliko ya hali ya hewa huko Alaska, ambako theluji kubwa kubwa inaanza kuyayuka, momonyoko wa maeneo ya Pwani na vijiji vinazama baharini.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Barack Obama wa Marekani amewahimiza viongozi wa dunia kuchukua hatua zinazo hitajika, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani wakati wa kikao cha kufungua mkutano wa viongozi wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mjini Paris.

Rais Obama alisisitiza kwamba dunia nzima hivi sasa iko katika hali ya dharura kuchukua hatua za kuzuia uchafuzi wa hewa kwa gezi za sumu na kupunguza kupanda kwa joto duniani.

Alisema ameshuhudia binafsi athari za mabadiliko ya hali ya hewa huko Alaska, ambako theluji kubwa kubwa inaanza kuyayuka, momonyoko wa maeneo ya Pwani na vijiji vinazama baharini

Obama alisema, Ilikua ni kushuhudia moja wapo ya uwezekano wa kitakachotokea, kuona kidogo hatima ya watoto wetu ikiwa hali ya hewa itaendelea kubadilika haraka kuliko juhudi zetu za kukabiliana nayo, yani mataifa kuzama miji kuhamwa ardhi kutoweza kuzailisha mavuna tena, mafuriko zaidi na watu kutafuta hifadhi katika mataifa mengine.

Viongozi wengine walozungumza jana wamesisitiza haja ya kufikiwa makubaliano baada ya wiki mbili za majadiliano wakisema hawataki kushuhudia yaliyotokea Copenhagan walipokutana miaka 6 iliyopita na kushindwa kufikia makubaliano.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ametoa wito kwa viongozi wa dunia kuharakisha hatua zinazohitajika kuzuia kuongezeka kwa hali ya joto.

Bw. Ban alisema, ukurasa unabidi kubadilika mjini paris kwa kuchukuliwa uwamuzi muhimu. Tunabidi kuiarifu dunia kwamba tunaelekea katika kupunguza uchafuzi wa mazingirana hakuna kurudi nyuma. Mipango ya kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa iliyoweasilishwa na zaidi ya mataifa 180 hii leo inahusiana na karibu asili mia mia moja ya matatizo ya uchafuzi wa hewa. Ni mwanzo mwema lakini inabidi twende kwa kasi zaidi.

Wanasayansi wanasema ikiwa watashindwa kukubaliana juu ya hatua thabiti huko Paris basi dunia itakumbwa na maafa makubwa ya kuongezeka kwa joto duniani itakayosababisha vimbunga vikali zaidi, ukame wa mara kwa mara na viwango vya bahari kuongezeka wakati barafu inayayuka katika maeneo ya kaskazini na kusini ya dunia.

XS
SM
MD
LG