Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:42

Benki Kuu yazifunga benki tano Tanzania


Bank Kuu Tanzania
Bank Kuu Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifutia leseni za biashara benki tano nchini na kuziweka chini ya mufilisi.

Pia BoT imetoa kikomo cha miezi sita kwa benki nyingine tatu kutekeleza masharti ya kisheria.

Kwa mujibu wa BoT imeeleza hatua hiyo iko ndani ya mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2)(a), (b) na (d), 58(2)(i),11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Shera ya Mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa benki zilizofutiwa leseni na kuwekwa chini ya mufilisi ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited.

Benki zilizopewa muda wa miezi sita kukidhi matwaka ya kisheria ni Benki ya Chama cha Ushirika Kilimanjaro, Benki ya Wanawake (TWB) na Tandahimba Community Bank.

Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu namba 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, BoT imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kuwa mfilisi kuanzia Januari 4, mwaka huu.

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake,” imeeleza taarifa iliyonukuliwa na vyombo vya habari.

Imeeleza upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.

XS
SM
MD
LG