Msemaji wa familia ya Clinton alisema moto huo ulikuwa kwenye nyumba iliyotumiwa na maafisa wa kitengo cha ujasusi cha Secret Service, na wala siyo nyumba ambamo rais huyo wa zamani na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton wanaishi.
Rais Clinton na mkewe hawakuwemo wakati wa kisa hicho na msemaji wao alieleza kuwa "kila kitu kiko shwari."
Familia hiyo inaishi katika kitongoji cha Chappaqua, mji wa New Castle, takriban Kilomita 64 Kaskazini Mashariki mwa mji wa New York.
Chanzo cha moto huo hakijkujulikana mara moja.