Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 15:49

Baraza la mpito la Haiti lachagua Waziri Mkuu mpya


Bango lenye picha ya Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Alix Didier Fils-Aime.
Bango lenye picha ya Waziri Mkuu mpya wa Haiti, Alix Didier Fils-Aime.

Baraza la mpito la Haiti, ambalo liliundwa ili kurejesha mfumo wa demokrasia nchini humo,  Jumapili limetia saini amri ya kiutendaji ya kumfuta  kazi kaimu waziri mkuu Garry Conille, na kuteuwa mfanyabiasha Alix Didier Fils-Aime, ambaye awali aliitaka kazi hiyo, kuchukua nafasi yake.

Amri hiyo itakayochapishwa Jumatano ilionyeshwa kwa shirika la habari la AP na vyanzo vya serikali. Hatua hiyo huenda ikaongeza matatizo kuelekea utawala wa kidemokrasia kwa Haiti ambayo haujakuwa na uchaguzi wa kidemokrasia kwa miaka mingi, sababu kuu ikiwa ghasia kutoka kwa makundi ya megenge.

Baraza la mpito lilibuniwa Aprili, likitwikwa jukumu la kuchagua waziri mkuu mpya, pamoja na baraza la mawaziri kwa matumaini ya kutuliza hali kwenye taifa hilo la Caribbean. Hata hivyo baraza hilo limegubikwa na siasa pamoja na migogoro, wakati baadhi ya wanachama wake wakituhumiwa kuhusika kwenye ufisadi mwezi uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG