Zaidi ya watu 10,000 nchini Haiti wamekimbia makazi yao ndani ya wiki iliyopita huku magenge yenye silaha yanayoendesha shughuli zake ndani na karibu na mji mkuu Port-au-Prince yakizidisha mashambulizi katika maeneo ambayo bado hayajadhibiti, kulingana na makadirio ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji siku ya Alhamisi.
Shirika hilo lilisema mwanzoni mwa Septemba kwamba zaidi ya watu 700,000 walikuwa wakimbizi wa ndani katika taifa hilo la Caribean, karibu mara mbili ya idadi ya miezi sita kabla.
Magenge katika wiki iliyopita yamekuwa yakizidisha mashambulizi kwenye miji kadhaa nje ya mji mkuu, ambapo sehemu kubwa ya jiji hilo na vitongoji vyake viko chini ya udhibiti wa makundi mbalimbali katili yenye silaha yaliyoungana chini ya muungano wa pamoja unaojulikana kama Viv Ansanm.
Forum