Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:47

Marekani : May athibitisha kujiuzulu kwa Balozi Darroch


Balozi Kim Darroch
Balozi Kim Darroch

Balozi wa Uingereza nchini Marekani Kim Darroch ametangaza kujiuzulu Jumatano, akisema ni vigumu kwake kuendelea kutumikia katika wadhifa wake kufuatia kuvuja kwa taarifa za kidiplomasia zilizokuwa na ukosoaji wake dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Katika barua ya kujiuzuli kwake Jumatano, Darroch amesema ingawaje wadhifa wake huo ulikuwa umalizike mwisho wa mwaka 2019, anaamini “hali ilivyokuwa hivi sasa mwelekeo wa uwajibikaji ni kuruhusu kuteuliwa balozi mpya.”

Alikuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza tangu mwaka 2016.

Darroch katika kumkosoa Trump ilikuwa pamoja na kumuelezea kiongozi huyo wa Marekani kama ni mtu "asiyemudu madaraka yake", "asiyejiamini" na "asiyekuwa na uwezo wa uongozi" na serikali yake “kwa njia ya kipekee haifanyi kazi.”

Taarifa hizo zilizovujishwa zilikuwa zinapelekwa kwa maafisa wa ngazi ya juu wa Uingereza. Wachunguzi wanaamini kuwa aliyevujisha habari hizo atapatikana na atakuwa ni kati ya wanasiasa wa Uingereza na siyo serikali ya kigeni.

Akizungumza katika Bunge la Uingereza Jumatano, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amethibitisha kujiuzulu kwa Darroch.

Trump alijibu kuvuja kwa taarifa hizo katika akaunti yake ya Twitter kwa kumuita Darroch “mtu mpuuzi sana” na “mpumbavu mwenye kiburi,” na kusema “hatafanya kazi tena” naye.

XS
SM
MD
LG