Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:33

AU yasema viongozi wa Afrika wamekasirishwa na kauli ya Trump


Balozi Arikana Chihombori-Quao,
Balozi Arikana Chihombori-Quao,

Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani, Arikana Chihombori-Quao, ameiambia VOA kuwa viongozi wa Afrika wamekasirishwa na tamko la udhalilishaji juu ya wahamiaji kutoka bara la Afrika na Haiti linalodaiwa kutolewa na Rais Donald Trump.

Amesema anategemea hatua zaidi rasmi na juhudi za kidiplomasia kupinga hilo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mabalozi wa Afrika kususia kuhudhuria hotuba ya rais ya hali ya taifa la Marekani kwenye Bunge la Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Heather Nauert amesema Marekani ina uhusiano imara na Waafrika na Haiti, uhusiano imara zaidi kuliko maoni yoyote, ameripoti mwandishi wa VOA.

Wakati hisia hasi zikiendelea kutolewa nchini Marekani na nchi za nje kutokana na kauli ambayo vyanzo kadhaa vimesema kuwa rais alitoa tamko juu ya aina ya wahamiaji anaopendelea waingie nchini Marekani, rais aliulizwa na mwandishi iwapo anataka wahamiaji zaidi watoke kutoka Norway.

Trump alijibu: “Nataka watoke kote ulimwenguni.

Msemaji wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amekiri kuwa rais alitumia lugha kali wakati wa mkutano wake na wabunge juu ya suala la wahamiaji, na kusema kuwa ni sehemu ya wito wake.

“Nafikiri kuwa hiyo ni moja ya sababu watu wa Marekani wanampenda Trump, sababu mojawapo iliyopelekea kushinda uchaguzi na anaendelea kuwepo katika ofisi yake ya Oval ya ikulu ya White House. Hii ni kwa sababu yeye sio mtu anayetegemea kuandikiwa kila kitu. Yeye ni mtu ambaye anaeleza vitu vile vilivyo mara nyingi, na mara nyingine anatumia lugha kali sana,” amesema Sanders.

Matokeo ya kauli hiyo yenye utata anayodaiwa kuitoa Trump, Botswana, Ghana, Haiti, Namibia, Senegal na Umoja wa Afrika wamepeleka malalamiko yao rasmi ya kidiplomasia kupiga udhalilishaji huo.

Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani, Arikana Chihombori-Quao ameiambia VOA kuwa matamko hayo hasi juu ya Afrika na Uongozi wa Trump wa sera ya “Marekani Kwanza” ni kimbingamizi kwa uhusiano wa muda mrefu wa karibu kati ya Marekani na bara la Afrika.

XS
SM
MD
LG