Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:44

Askari wa vikosi maalum vya Marekani auawa Somalia


Vikosi vya majeshi ya majini vya Marekani nchini Somalia
Vikosi vya majeshi ya majini vya Marekani nchini Somalia

Wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia wamemua askari wa vikosi maalumu vya Marekani Ijumaa na kuwajeruhi wengine watatu katika kikosi hicho kinachowasaidia wanajeshi wa Somalia, maafisa wa Marekani wamesema.

Mpiganaji huyo wa jeshi la majini (Navy Seal) aliyeuawa katika operesheni dhidi ya al-Shabab alikuwa askari wa kwanza wa Marekani kupatwa na janga hilo katika nchi iliyokumbwa na vita tangu mapigano makali yalivyotokea mwaka 1993—mapambano yaliyohamasisha kutengenezwa kwa filamu ya Black Hawk Down.

Maafisa wa Ikulu ya White House wamesema Rais Donald Trump ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya wahanga hao, pamoja na kueleza kuridhishwa kwake na juhudi za wanajeshi hao kati yao wakiwemo wanaume na wanawake.

Silaha ndogo iliotumika kurusha risasi ilimua Navy Seal huyo katika kijiji kidogo kilichopo kilometer 65 magharibi ya Mogadishu. Afisa wa Jeshi la Marekani ameiambia Sauti ya Amerika (VOA) kwamba sio chini ya askari wa Navy Seal wawili na mkalimani wao walijeruhiwa katika shambulizi hilo katika kijiji cha Barire, Magharibi ya Afgoye.

Kikosi cha Africa Command, kilichokuwa na jukumu la usimamizi wa operesheni zote za jeshi la Marekani katika bara la Afrika, kimesema kuwa majeshi ya Marekani yalishambuliwa katika harakati za jeshi hilo kuwa likiwashauri na kuwasaidia bega kwa bega wanajeshi wa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA).

“Hii ilikuwa ni katika kutekeleza majukumu yao nchini Somalia,” msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Kapteni wa jeshi la Majini Jeff Davis amewaambia waandishi siku ya Ijumaa.

Vikosi vya Marekani vilikuwa katika operesheni ya kusaidia majeshi ya SNA katika shambulio lililokuwa limelenga eneo linalohusishwa na matukio ya mashambulizi karibu na vituo vinavyotumiwa na majeshi ya Marekani na Somalia, amesema.

Afisa wa ngazi ya juu wa mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia amesema askari walivamia jengo la Radio Andalus, ambacho ni kituo rasmi cha al-Shabab.

Shambulio hilo liliua wapiganaji wa al-Shabab nane, afisa huyo amesema, akiongeza kuwa vifaa vya kituo hicho cha radio vimeripotiwa kukamatwa.

“Tuliwasaidia kuwaleta wanajeshi wa Somalia kwa kutumia ndege zetu, na sisi tulikuwa tuko mbali nyuma kabisa wakati wakiendelea na operesheni hiyo dhidi ya al-Shabab,” Davis amesema akiwa Wizara ya Ulinzi Marekani. “Hapo ndipo majeshi yetu yaliposhambuliwa.”

XS
SM
MD
LG