Katika eneo la wachimbaji wa Australia nchini angola, wameitaja almasi ya karati 170 Lulo Rose.
Wamesema almasi hiyo itauzwa katika mashirika ya kimataifa na kampuni ya masoko ya almasi ya Angola.
Upatikanaji huo umekaribishwa na serikali ya Angola. “Rekodi hii ya almasi ya waridi iliyopatikana katika Lulo inazidi kuonyesha Angola kama nchi muhimu duniani katika machimbo ya almasi.”
Waziri wa madini Diamantino Azevedo amenukuliwa akisema katika taarifa kwamba jiwe kama hilo limewahi kuuzwa kwa bei ya kubwa sana.
Lilikuwa jiwe la rangi ya waridi lenye karati 59 liliuzwa kwa dola milioni 71.2 mwaka 2017 ikiwa ni bei ya juu kuwahi kutokea.