Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:48

Al-shabab yadai kuhusika na shambulizi jingine Somalia


Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia.
Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia.

Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia wanadai kuhusika na shambulizi moja ambalo lilimlenga kiongozi muhimu wa kisiasa nchini humo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanane.

Sharif Hassan Sheikh Aden
Sharif Hassan Sheikh Aden

Shambulizi hilo la Alhamis katika mji wa Baidoa lililenga makazi rasmi na makao makuu ya Sharif Hassan Sheikh Aden, spika wa zamani wa bunge la Somalia na hivi sasa ni mkuu wa jimbo la South Western nchini Somalia.

Mashahidi walisema wanamgambo walitegua bomu la kwenye gari nje ya makazi na kisha walifyatua risasi na kusababisha mapambano na walinzi.

Kamishna wa polisi wa eneo aliiambia Idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika-VOA kwamba watu 12 waliuwawa lakini maafisa kadhaa katika eneo hilo baadae walieleza kuwa idadi ya vifo ni watu wanane, ikiwemo washambuliaji watatu, wanajeshi watatu wa kisomali na wanajeshi wawili wa Ethiopia waliopo katika jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia-AMISOM.

Spika wa zamani wa bunge, Aden inasemekana kuwa yupo salama na hajajeruhiwa.

Al Shabab pia walishambulia makazi ya Rais wa Somalia
Al Shabab pia walishambulia makazi ya Rais wa Somalia

Tovuti zinazounga mkono al-Shabab ziliripoti kundi hilo kuhusika na shambulizi haraka baada ya shambulizi kufanyika.

Shambulizi hilo lilikuwa linafanana na mashambulizi mengine ya hivi karibuni yanayofanywa na kundi lenye uhusiano na al-Qaida ambalo limeongeza mashambulizi ya kuwalenga maafisa wa serikali. Kundi la al-Shabab linadai kuhusika kwa kuwauwa wabunge sita tangu mwanzoni mwa mwaka 2014 na kufanya mashambulizi mawili ya bomu pamoja na bunduki kwenye makazi ya rais mwaka jana.

AMISOM ilisema Alhamis kuwa mashambulizi ni majaribio ya kukata tamaa yanayofanywa na kundi la al-Shabab linalosaka umhimu kufuatia kushindwa na majeshi ya AMISOM na jeshi la taifa la Somalia.

XS
SM
MD
LG